Fasteey POS - Mfumo wa Mauzo Android

Fasteey POS - Mfumo wa Mauzo

POS app ya Tanzania: mauzo, stoki, ripoti na matawi mengi kwenye simu moja
Downloader for Instagram
Looking to download Instagram videos? Try:

Overview

Features & Capabilities

Fasteey POS ni POS app ya kisasa kwa wafanyabiashara wa Tanzania. Simamia mauzo, stoki, wateja, wasambazaji na ripoti za duka lako kwenye simu moja - bila daftari, bila stress.

Una duka moja au matawi mengi? Fasteey POS ni cloud POS system yenye AI Assistant inayokusaidia kujua faida yako halisi, stoki inayokwisha na tawi lipi linafanya vizuri - kila siku, popote ulipo.

INAFAA KWA BIASHARA GANI?
• Duka la rejareja na mini-supermarket
• Duka la jumla (wholesale)
• Pharmacy na duka la dawa
• Salon, barbershop na spa
• Restaurant, cafe, juice bar na bakery
• Boutique, nguo na viatu
• Hardware na vifaa vya ujenzi
• Spare parts, simu na electronics
• Agrovet na biashara za vyakula
• Biashara yenye matawi mengi

VIPENGELE VIKUU

✔ Mauzo (Sales)
Fanya mauzo kwa haraka na uone mauzo ya siku, wiki au mwezi papo hapo. Kila mauzo yanarekodiwa kiotomatiki.

✔ Stoki na Inventory Control
Sajili bidhaa zako, weka bei, na ufuatilie stoki kwa wakati halisi. Pata tahadhari stoki ikipungua au bidhaa ikikaribia kuisha muda (expiry alerts). Rekodi uhamisho wa bidhaa kati ya matawi, bidhaa zilizorudishwa (returns) na zilizoharibika (damages).

✔ Manunuzi na Wasambazaji
Rekodi manunuzi, ongeza stoki, na ufuatilie madeni ya wasambazaji wako.

✔ Wateja na Madeni
Hifadhi taarifa za wateja wako, historia ya manunuzi yao na salio wanalodaiwa.

✔ Matumizi, Mapato na Akaunti
Rekodi matumizi ya biashara, angalia mapato yako, na ufuatilie fedha zinazoingia na kutoka benki.

✔ Ripoti za Biashara
Ripoti za mauzo, stoki na fedha zinazoweza kuchapishwa. Jua faida yako halisi kabla ya kufanya maamuzi.

✔ Wafanyakazi na Ruhusa
Ongeza wafanyakazi na uwape ruhusa kulingana na kazi zao. Tumia Activity Logs kuona nani alifanya nini na lini.

✔ Matawi Mengi (Multi-Store)
Simamia matawi yote ya biashara yako kutoka dashboard moja.

✔ Arifa Mahiri (Smart Notifications)
Pata taarifa za mauzo kwa wakati halisi kupitia WhatsApp, SMS, Email, Telegram au Slack.

✔ AI Assistant
Ongea na mfumo wako kama unavyochat na msaidizi wa biashara na upate majibu ya haraka kuhusu mauzo, faida na stoki. Mfano: "Bidhaa gani iliuza zaidi wiki hii?"

KWA NINI FASTEEY POS?
• Acha daftari na Excel - kila kitu kiko kwenye app moja.
• Jua faida halisi, sio mauzo tu.
• Dhibiti stoki na punguza hasara ya bidhaa zinazopotea au kuharibika.
• Simamia wafanyakazi na matawi hata ukiwa mbali na duka.
• Imetengenezwa Tanzania, kwa wafanyabiashara wa Tanzania.

ANZA BURE
Anza na Free Plan, kisha chagua mpango wa kulipia ukiwa tayari kufungua vipengele vyote - kwa mwezi 1, miezi 3, miezi 6 au mwaka 1.

JINSI YA KUANZA
1. Pakua Fasteey POS na utengeneze akaunti (kwa fomu au Gmail).
2. Sajili biashara yako na bidhaa zako.
3. Anza kuuza na kufuatilia faida yako.

MAFUNZO NA MSAADA
Tuna video za mafunzo za Kiswahili kwenye YouTube (tafuta "Fasteey POS") zinazokuonyesha kila hatua.
Website: fasteeypos.com
Instagram: @fasteey___
TikTok: @fasteey_

MASWALI YA KAWAIDA
Je, Fasteey POS inafaa duka dogo? Ndiyo. Unaweza kuanza na Free Plan hata ukiwa na duka moja.
Naweza kusimamia matawi zaidi ya moja? Ndiyo, kutoka akaunti moja.
Wafanyakazi wangu wanaweza kutumia? Ndiyo, kwa ruhusa unazowapa.
Inapatikana kwenye iPhone? Ndiyo, Fasteey POS inapatikana pia kwa iPhone.

Fasteey POS - point of sale system, inventory management, stock control na bookkeeping kwa duka, pharmacy, salon, restaurant na biashara yoyote Tanzania. Pakua leo na ukuze biashara yako.

Imetengenezwa na Intelfric Technology Limited, Dar es Salaam.

User Growth & Download Statistics

App
By:
INTELFRIC TECHNOLOGY LIMITED
Downloads:
47 18
Version:
0 Last updated: 2026-10-24
Creation date:
2026-10-24
Publisher country:
KR KR
Email:
co*****@gmail.com
Website:
Privacy policy:
Full description:
See detailed description
Source:
Google Play Store
Data ingested on:
2026-11-22
Compare stats and ranking:

Contact the developer

Chrome-Stats does not own this Android app. Please use these information below to contact the Android app developer.

Developed by:
INTELFRIC TECHNOLOGY LIMITED
Google Play Store
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.fasteey.pos
Email:
co*****@gmail.com
Website:
https://fasteeypos.com/

Best Fasteey POS - Mfumo wa Mauzo Alternatives

Here are some Android apps that are similar to Fasteey POS - Mfumo wa Mauzo: