Features & Capabilities

Masifu ni programu ya Liturujia ya Vipindi (Liturgy of the Hours) iliyoundwa maalum kwa lugha ya Kiswahili na Mashirika ya Klareti (Claretian International). Programu hii inakusaidia kusali sala rasmi za Kanisa Katoliki kila siku — asubuhi, mchana, na jioni — popote ulipo, hata bila mtandao. SALA ZA KILA SIKU Sala za Liturujia zimepangwa kwa mujibu wa kalenda ya liturujia — Zaburi, Antifonari, Usomaji Mfupi, na Maombi ya Mwisho — kwa nyakati zote tatu za siku.

WATAKATIFU WA SIKU Tazama mtakatifu anayekumbukwa leo pamoja na maelezo ya maisha yake. Angalia video za YouTube kuhusu watakatifu moja kwa moja ndani ya programu.

MISA TAKATIFU Fuata Misa Takatifu kamili kwa lugha ya Kiswahili, ikiwemo Ibada ya Siku ya Bwana Bila Padre, iliyoandaliwa kwa uangalifu. SALA ZINGINE • Rozari Takatifu • Litania za Watakatifu • Njia ya Msalaba (Via Crucis) • Sala za Kila Siku — Sala za Asubuhi, Jioni, Chakula, na zaidi • Sala kwa Mt. Antoni Maria Klareti

SOMA AU SIKILIZA Kila sala inaweza kusomwa kwenye skrini au kusikilizwa kwa sauti (Text-to-Speech) kwa Kiswahili. Badilisha ukubwa wa maandishi kulingana na upendeleo wako. MANDHARI MBILI Chagua kati ya mandhari ya giza (usiku) au mwanga (mchana) inayobadilika kulingana na wakati wa siku, au weka wewe mwenyewe.

INAFANYA KAZI BILA MTANDAO Maudhui yote ya sala na liturujia yanapatikana bila mtandao baada ya ku download programu. Sala zitapatikana ata unaposali mahali pasipo na mtandao.

KALENDA YA LITURUJIA Programu inafuata kalenda kamili ya liturujia ya Kanisa Katoliki — Majilio, Noeli, Kwaresma, Pasaka, na Wakati wa Kawaida — na kubadilisha rangi za liturujia ipasavyo.


Masifu imeundwa na Mashirika ya Klareti Tanzania kwa ajili ya Wakristo wanaotaka Inafaa kwa makasisi, watawa, waamini wa awali, vijana, na familia nzima.

Pakua Masifu leo na uanze siku yako na sala.

User Growth & Download Statistics

App
By:
MAGIGE CHARLES WESALILO
Version:
1.1 Last updated: 2026-04-26
Version code:
884919237
Creation date:
2026-03-28
Compatible devices:
Size:
45.03MB
URLs:
Privacy policy
Full description:
See detailed description
Source:
Apple Apps Store
Data ingested on:
2026-06-07
Compare stats and ranking:

Contact the developer

Chrome-Stats does not own this Apple app. Please use these information below to contact the Apple app developer.
Developed by:
MAGIGE CHARLES WESALILO
Apple Apps Store
https://apps.apple.com/ke/app/masifu-sala-ya-kanisa/id6761155004

Best Masifu - Sala ya Kanisa Alternatives

Here are some Apple apps that are similar to Masifu - Sala ya Kanisa: