Dukani - Simamia biashara yako Apple

Dukani - Simamia biashara yako

Biashara yako, mikononi mwako

Overview

Version:
3.0.2
Last updated: 2026-08-18
Ranking
#1,002,324 ▼ 1,862
Overall

Features & Capabilities

Dukani — Simamia biashara yako kwa uelewa zaidi

Dukani ni programu rahisi na salama ya kusimamia biashara, iliyoundwa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na wa kati Tanzania.

Iwe una duka la rejareja, grocery, kiosk, minimarket, jumla au biashara nyingine, Dukani inakusaidia kurekodi na kufuatilia shughuli muhimu za biashara yako kwa urahisi.

Jua mauzo yako, fuatilia bidhaa zako, simamia madeni na gharama, na pata picha nzuri ya biashara yako — hata ukiwa huna intaneti.

SIMAMIA BIASHARA YAKO

Dukani inakusaidia:

• Kurekodi mauzo kwa haraka • Kufuatilia bidhaa na stock • Kurekodi manunuzi na kuongeza stock • Kufuatilia wateja na wauzaji • Kusimamia mauzo ya mkopo na madeni • Kurekodi gharama za biashara • Kufuatilia bei ya kununua na kuuza • Kuona taarifa na ripoti za biashara yako

Fuatilia STOCK kwa urahisi

Jua bidhaa ulizonazo na jinsi stock yako inavyobadilika kutokana na mauzo, manunuzi na marekebisho.

Dukani pia inakusaidia kutumia vipimo tofauti kama:

  • Kipande
  • Box
  • Dozen
  • Kg
  • Lita na vipimo vingine kulingana na biashara yako.

ELEWA MAUZO NA FAIDA YAKO

Usiishie kujua umeuza kiasi gani.

Dukani hukusaidia kupata picha ya biashara yako kwa kutumia taarifa za mauzo, gharama na bidhaa zako.

Jua biashara yako vizuri zaidi na fanya maamuzi ukiwa na taarifa sahihi.

BIASHARA YENYE WAFANYAKAZI?

  • Dukani inaweza kusaidia biashara yenye wafanyakazi kusimamia shughuli za kila siku huku mmiliki akiwa na uelewa wa kinachoendelea kwenye biashara.
  • Mmiliki anaweza kufuatilia shughuli za biashara bila kutegemea taarifa za maneno pekee.

INAFANYA KAZI HATA BILA INTANETI

  • Huna internet muda wote? Hakuna tatizo.
  • Dukani imeundwa kufanya kazi hata wakati hakuna muunganisho wa internet. Unaweza kuendelea kurekodi mauzo na kusimamia taarifa za biashara yako.
  • Internet inapopatikana, taarifa husawazishwa na mfumo kulingana na utaratibu wa Dukani.

TAARIFA ZA BIASHARA YAKO

  • Taarifa za biashara yako huhifadhiwa kwenye kifaa chako na kusawazishwa na mfumo unapopatikana mtandao.
  • Hii inakusaidia kuendelea kufanya kazi hata maeneo yenye internet hafifu au isiyotabirika.

IMETENGENEZWA KWA MAHITAJI YA BIASHARA ZA TANZANIA

Dukani imejengwa kwa kuzingatia mazingira halisi ya biashara — kuanzia maduka madogo hadi biashara zinazokua.

Lengo ni moja:

Kukusaidia kuelewa biashara yako, kuisimamia vizuri na kufanya maamuzi bora.

ANZA LEO

Pakua Dukani, ongeza bidhaa zako na anza kurekodi biashara yako.

Dukani — Biashara yako, mikononi mwako.

User Growth & Download Statistics

App
By:
KAPPU FINTECH LIMITED
Version:
3.0.2 Last updated: 2026-08-18
Version code:
889922289
Creation date:
2026-01-08
Compatible devices:
Size:
48.65MB
URLs:
Website ,Privacy policy
Full description:
See detailed description
Source:
Apple Apps Store
Data ingested on:
2026-08-27
Compare stats and ranking:

Contact the developer

Chrome-Stats does not own this Apple app. Please use these information below to contact the Apple app developer.
Developed by:
KAPPU FINTECH LIMITED
Apple Apps Store
https://apps.apple.com/tz/app/dukani-simamia-biashara-yako/id6757365142
Website:
https://dukaniapp.com/

Best Dukani - Simamia biashara yako Alternatives

Here are some Apple apps that are similar to Dukani - Simamia biashara yako: