Features & Capabilities

Pata ushauri wa madaktari, tathmini ya afya kwa AI, afya ya akili, hedhi na ujauzito - yote ndani ya app moja. Inapatikana kwa Kiswahili na Kiingereza. Pakua TanzMED sasa

TanzMED – Afya Rahisi, Popote Ulipo

TanzMED ni jukwaa la kidijitali la afya linalounganisha madaktari, hospitali, maduka ya bidhaa za Afya na urembo, maabara, huduma za afya nyumbani, na zana za afya zinazotumia AI ndani ya programu moja salama.

TanzMED imeundwa kwa ajili ya Afrika Mashariki ili kufanya huduma bora za afya zipatikane kwa urahisi, gharama nafuu, na kwa wakati wowote.

Afya yako. Programu moja.

--> Ushauri wa Daktari Mtandaoni

Wasiliana na madaktari na wataalamu wa afya waliothibitishwa kupitia mazungumzo ya video za papo kwa hapo (Instant) au kwa miadi (Appointment). Pata ushauri wa kitaalamu, ufuatiliaji wa afya, na rufaa bila kwenda popote ulipo.

:::: Huduma za Afya Nyumbani ::::

Weka miadi ya wauguzi, madaktari, au walezi kwa huduma salama na za kitaalamu ukiwa nyumbani au ofisini, ikijumuisha ufuatiliaji wa afya na huduma za matibabu.

:::: Afya ya Akili ::::

Pata msaada wa afya ya akili kupitia mazungumzo ya siri na wataalamu. Tumia zana na huduma za usaidizi zinazolenga kuboresha ustawi wa kihisia na kisaikolojia.

:::: Tathmini ya Afya kwa Kutumia AI ::::

Eleza dalili zako na upate tathmini ya awali inayotumia teknolojia ya AI ili kukusaidia kuelewa hali yako na hatua inayofuata ya kuchukua.

:::: Afya ya Mama na Mtoto ::::

Fuatilia maendeleo ya ujauzito, ratiba za chanjo, ukuaji wa mtoto, na upate ushauri wa wataalamu wa afya ya mama na mtoto.

:::: Afya ya Mwanamke ::::

Dhibiti mzunguko wa hedhi, uzazi, na afya ya uzazi. Pata msaada na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ya wanawake kupitia programu.

:::: Jamii ya Afya (Kijiwe cha Afya) ::::

Uliza maswali ya afya, shiriki katika mijadala, fuatilia mada za wataalamu wa afya, na jifunze kutoka kwa jamii inayojali afya. Ushiriki wa faragha unapatikana pale inapohitajika.

:::: Dawa na Vipimo vya Maabara ::::

Agiza bidhaa za Afya mtandaoni, weka miadi ya vipimo vya maabara, na pata huduma kutoka kwa maduka ya dawa na maabara zilizo karibu nawe.

:::: Elimu na Makala za Afya ::::

Soma makala za afya zilizoandikwa na kuthibitishwa na wataalamu, zinazojadili magonjwa ya kawaida, kinga, mtindo bora wa maisha, na ustawi wa afya kwa ujumla.

:::: Miadi ya Hospitali na Wataalamu ::::

Pata urahisi wa kuweka miadi na hospitali, maabara, na madaktari bingwa kupitia programu ya TanzMED.

Imejengwa kwa Uaminifu na Usalama

TanzMED imeundwa kwa kuzingatia usalama wa taarifa binafsi, faragha, na urahisi wa matumizi. Programu inapatikana kwa Kiswahili na Kiingereza ili kuwafikia watumiaji wengi zaidi Afrika Mashariki.

:::: Kanusho la Kitabibu ::::

TanzMED haitoi utambuzi rasmi wa magonjwa na haichukui nafasi ya ushauri au huduma za kitaalamu kutoka kwa mtaalamu wa afya. Kwa dharura za kiafya, tafadhali wasiliana na huduma za afya za karibu mara moja.

User Growth & Download Statistics

App Mature
By:
Africa Healthtech Limited
Rating:
5.00
(2)
Version:
7.0.16 Last updated: 2026-05-26
Version code:
886021314
Creation date:
2024-07-19
Compatible devices:
Size:
214.93MB
URLs:
Website ,Privacy policy
Full description:
See detailed description
Source:
Apple Apps Store
Data ingested on:
2026-06-03
Compare stats and ranking:

Contact the developer

Chrome-Stats does not own this Apple app. Please use these information below to contact the Apple app developer.
Developed by:
Africa Healthtech Limited
Apple Apps Store
https://apps.apple.com/us/app/tanzmed-afya-kiganjani/id6505112947
Website:
https://www.youtube.com/watch?v=1l1D9XNdnXs

User Reviews

Very great app, with a brilliant UI and very easy to use
by Ab*****, 2025-12-20
View all user reviews ›

Best TanzMED - Afya Kiganjani Alternatives

Here are some Apple apps that are similar to TanzMED - Afya Kiganjani: