# Fundi Kiganjani

> Pata huduma sahihi kwa haraka.

Canonical page: [https://chrome-stats.com/d/id6770313261](https://chrome-stats.com/d/id6770313261)

## Overview

- **ID:** `id6770313261`
- **Platform:** Apple
- **Type:** Apple app
- **Status:** Available
- **Publisher:** ELLEANNA CONSTRUCTION LTD
- **Category:** Lifestyle
- **Version:** 1.2.0
- **Last updated:** 2026-07-13
- **First published:** 2026-07-13
- **Size:** 45 MB
- **Data as of:** 2026-09-22
- **Store listing:** [Apple App Store](https://apps.apple.com/tz/app/fundi-kiganjani/id6770313261)
- **Website:** [https://fundikiganjani.com](https://fundikiganjani.com/)
- **Privacy policy:** [https://fundikiganjani.com/privacy](https://fundikiganjani.com/privacy)

## Description

Pata huduma za kuaminika karibu nawe fundi bomba, umeme, AC, urembo na zaidi. Mazungumzo ndani ya app na ufuatiliaji wa moja kwa moja.

Fundi Kiganjani: pata huduma sahihi, kwa haraka.

Andika tatizo lako au pitia kategori na tutakuonyesha mafundi waliothibitishwa walio karibu na wewe ndani ya Tanzania. Mazungumzo na watoa huduma pamoja na ufuatiliaji vyote vinafanyika ndani ya app.

KWA WATEJA

• Tafuta kwa kuelezea tatizo au kuchagua kategoria. mf. bomba la maji linavuja, AC haifanyi kazi, soketi imeungua, n.k.
• Linganisha watoa huduma walioko karibu nawe kwa ujuzi, eneo, n.k.
• Tuma maombi kwa watoa huduma moja kwa moja: anayefaa zaidi atapokea taarifa.
• Mazungumzo ndani ya app, picha na maelezo yote yanabaki pamoja na ombi.
• Fuatilia fundi moja kwa moja kwenye ramani ona anavyokukaribia na hatua ya kazi.
• Pokea arifa kila kwa hatua: mf. ombi limekubaliwa, fundi yuko njiani, fundi amefika.
• Hakiki fundi na uone maoni ya wateja waliopita.
• Hifadhi anwani za nyumbani, kazini, na mahali pengine.

KWA WATOA HUDUMA

• Jenga wasifu wa kitaalamu unaoelezea huduma, ujuzi, miaka ya uzoefu, na picha za kazi.
• Weka eneo la huduma na saa zako za kazi.
• Pokea ombi kutoka wateja walio karibu nawe moja kwa moja.
• Kubali au kataa maombi kwa haraka.

HUDUMA TUNAZOFIKISHA

• Umeme — wiring, solar, generata, AC, vifaa vya umeme
• Bomba na Maji — mabomba, mifereji, pampu, matanki
• Vifaa vya Elektroniki — simu, kompyuta, TV, friji
• Magari na Usafiri — magari, pikipiki, bodaboda
• Ujenzi na Ukarabati — useremala, uashi, rangi, vigae, paa
• Mahitaji ya Nyumbani — usafi, kufua, upishi
• Urembo na Vipodozi — nywele, kucha, ngozi, masaji
• Ufundi wa Kipekee — vito, saa, sanaa za mikono

KWA NINI FUNDI KIGANJANI

• Mafundi waliothibitishwa kila wasifu unakaguliwa na timu yetu.
• Maoni ya kweli kutoka wateja waliopita.
• Lugha mbili,Kiswahili na Kiingereza.

Pakua Fundi Kiganjani leo.

## Rankings

- #1,683,564 — Overall

## Similar extensions and apps

- [SOKO by tunzaa](https://chrome-stats.com/d/id1578263762) — 5.00 / 5
- [MWINYI App](https://chrome-stats.com/d/id6670269540)
- [Ndinga App](https://chrome-stats.com/d/id6758467495)
- [Napa Mobile App](https://chrome-stats.com/d/id1627224691) — 3.00 / 5
- [TanzMED - Afya Kiganjani](https://chrome-stats.com/d/id6505112947) — 4.60 / 5
- [WCF Mkononi](https://chrome-stats.com/d/id6747836446)
- [Wakala Digital](https://chrome-stats.com/d/id1629185156)
- [SAMIA App](https://chrome-stats.com/d/id6497486238) — 4.00 / 5
- [WakiliApp](https://chrome-stats.com/d/id1590337837)

---

Source: [Chrome-Stats](https://chrome-stats.com/d/id6770313261)
