# Dukani - Simamia biashara yako

> Biashara yako, mikononi mwako

Canonical page: [https://chrome-stats.com/d/id6757365142](https://chrome-stats.com/d/id6757365142)

## Overview

- **ID:** `id6757365142`
- **Platform:** Apple
- **Type:** Apple app
- **Status:** Available
- **Publisher:** KAPPU FINTECH LIMITED
- **Category:** Business
- **Version:** 3.5.0
- **Last updated:** 2026-09-17
- **First published:** 2026-01-08
- **Size:** 55 MB
- **Data as of:** 2026-09-18
- **Store listing:** [Apple App Store](https://apps.apple.com/tz/app/dukani-simamia-biashara-yako/id6757365142)
- **Website:** [https://dukaniapp.com/](https://dukaniapp.com/)
- **Privacy policy:** [https://dukaniapp.com/privacy-policy/](https://dukaniapp.com/privacy-policy/)

## Description

Dukani — Simamia biashara yako kwa uelewa zaidi

Dukani ni programu rahisi na salama ya kusimamia biashara, iliyoundwa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na wa kati Tanzania.

Iwe una duka la rejareja, grocery, kiosk, minimarket, jumla au biashara nyingine, Dukani inakusaidia kurekodi na kufuatilia shughuli muhimu za biashara yako kwa urahisi.

Jua mauzo yako, fuatilia bidhaa zako, simamia madeni na gharama, na pata picha nzuri ya biashara yako — hata ukiwa huna intaneti.

SIMAMIA BIASHARA YAKO

Dukani inakusaidia:

• Kurekodi mauzo kwa haraka
• Kufuatilia bidhaa na stock
• Kurekodi manunuzi na kuongeza stock
• Kufuatilia wateja na wauzaji
• Kusimamia mauzo ya mkopo na madeni
• Kurekodi gharama za biashara
• Kufuatilia bei ya kununua na kuuza
• Kuona taarifa na ripoti za biashara yako

Fuatilia STOCK kwa urahisi

Jua bidhaa ulizonazo na jinsi stock yako inavyobadilika kutokana na mauzo, manunuzi na marekebisho.

Dukani pia inakusaidia kutumia vipimo tofauti kama:
- Kipande
- Box
- Dozen
- Kg
- Lita
na vipimo vingine kulingana na biashara yako.

ELEWA MAUZO NA FAIDA YAKO

Usiishie kujua umeuza kiasi gani.

Dukani hukusaidia kupata picha ya biashara yako kwa kutumia taarifa za mauzo, gharama na bidhaa zako.

Jua biashara yako vizuri zaidi na fanya maamuzi ukiwa na taarifa sahihi.

BIASHARA YENYE WAFANYAKAZI?

- Dukani inaweza kusaidia biashara yenye wafanyakazi kusimamia shughuli za kila siku huku mmiliki akiwa na uelewa wa kinachoendelea kwenye biashara.
- Mmiliki anaweza kufuatilia shughuli za biashara bila kutegemea taarifa za maneno pekee.

INAFANYA KAZI HATA BILA INTANETI

- Huna internet muda wote? Hakuna tatizo.
- Dukani imeundwa kufanya kazi hata wakati hakuna muunganisho wa internet. Unaweza kuendelea kurekodi mauzo na kusimamia taarifa za biashara yako.
- Internet inapopatikana, taarifa husawazishwa na mfumo kulingana na utaratibu wa Dukani.

TAARIFA ZA BIASHARA YAKO

- Taarifa za biashara yako huhifadhiwa kwenye kifaa chako na kusawazishwa na mfumo unapopatikana mtandao.
- Hii inakusaidia kuendelea kufanya kazi hata maeneo yenye internet hafifu au isiyotabirika.

IMETENGENEZWA KWA MAHITAJI YA BIASHARA ZA TANZANIA

Dukani imejengwa kwa kuzingatia mazingira halisi ya biashara — kuanzia maduka madogo hadi biashara zinazokua.

Lengo ni moja:

Kukusaidia kuelewa biashara yako, kuisimamia vizuri na kufanya maamuzi bora.

ANZA LEO

Pakua Dukani, ongeza bidhaa zako na anza kurekodi biashara yako.

Dukani — Biashara yako, mikononi mwako.

Terms of Use (EULA): https://www.apple.com/legal/internet-services/itunes/dev/stdeula/
Privacy Policy: https://dukaniapp.com/privacy-policy

## Rankings

- #1,008,957 — Overall

## Similar extensions and apps

- [Duka Pro](https://chrome-stats.com/d/id6792279821)
- [Biashara Kiganjani](https://chrome-stats.com/d/id6777196067)
- [Selpoa](https://chrome-stats.com/d/id6479444616)
- [RINO: Mfumo wa Biashara](https://chrome-stats.com/d/id6757956022) — 5.00 / 5
- [Wakala Digital](https://chrome-stats.com/d/id1629185156)
- [myDuka: Manage Your Shop](https://chrome-stats.com/d/id6783097232)
- [DuukaMobile](https://chrome-stats.com/d/id6761978325)
- [aje farms](https://chrome-stats.com/d/id6738954741)
- [Tunzaa Plus](https://chrome-stats.com/d/id1596907284)
- [myDuka: Online Shopping](https://chrome-stats.com/d/id6783598770)

---

Source: [Chrome-Stats](https://chrome-stats.com/d/id6757365142)
